Loading...
 

Mashindano ya Hotuba za Kielimu

 

Education

 

Muda wa Hotuba

Mashindano ya Hotuba za Kielimu yana lengo la kutafuta watu wenye mawasiliano mazuri ya kisayansi ambao wanaweza kuangaza, kuhamasisha, na kufundisha watu.

Hotuba zinazoingia kwenye Mashindano ya Hotuba za Kielimu lazima ziwe na muda wa usiozidi dakika 10.

Mada za Hotuba

Mada za Mashindano ya Hotuba za Kielimu lazima ziwe kutoka sayansi rasmi, asili au ya kijamii.

Maudhui ya hotuba yanatakiwa kulingana na hali ya sayansi iliyokubaliwa kama ilivyoeleweka na jamii ya watafiti waliochapisha kwenye jarida linalotambuliwa na watafiti wengine.

Washiriki ambao wanawasilisha hotuba kuhusu mada za sayansi ya uwongo au mada ambazo sio zilizotajwa hapo juu wataondolewa.

Uchaguzi wa Majaji

Kwa mashindano ya ngazi ya nchi na juu, majaji watakuwa sio wanachama wa Agora, ambao watakuwa kutoka taaluma zifuatazo:

  • Wataalam wa vyombo vya habari - watangazaji, watangazaji wa vipindi, waigizaji, watayarishaji, nk., kutoka runinga, redio, magazeti, au filamu.
  • Maprofesa wa shule au chuo kikuu.
  • Waandishi wa habari
  • Wakurugenzi wa makampuni ya saizi ya kati na makubwa.
  • Wazungumzaji wataalam kutoka mzunguko wa uzungumzaji wa mbele ya hadhira (wanaolipwa).
  • Wazungumzaji kutoka matukio mengine ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira kama vile TEDx., Munk Debates, nk.


Alama za Hotuba

Majaji watatoa alama za hotuba kulingana na vigezo vifuatavyo:

  • Uwazi na uzingatiifu (0 mpaka 10) - Watazingatia kama hotuba ilikuwa ya wazi, lenye lengo moja la kielimu
  • Utumiaji wa zana au visaidizi vya kuona (0 mpaka 10) - Watazingatia kama utumiaji wa zana / visaidizi vya kuona vilifaa na uhalisia.
  • Usahihi wa kisayansi (0 mpaka 10) - Watazingatia ukaribu wa hotuba na uelewa wa mada ya sasa ya kisayansi ya hotuba ambayo imewasilishwa.
  • Utoshelevu kwa hadhira ya kawaida (0 mpaka 10) - Watazingatia jinsi gani hadhira ya kawaida imeelewa hotuba.
  • Ubora na uvutiaji wa hotuba kwa ujumla (0 mpaka 10) - Watazingatia jinsi gani hotuba imeburudisha, kama iliweza kukamata na kushikilia umakini wa wasikilizaji.

Kwa kila hotuba, wastani wa kila alama za hapo juu utatafutwa, na hiyo ndio itakuwa alama ya mwisho atakayopewa mshiriki.

Cheo

Mshindi wa ngazi yoyote ile isipokuwa Fainali za Dunia atakuwa na cheo cha "Mzungumzaji Bora wa Kielimu wa (kanda)"     

 


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Saturday August 21, 2021 07:48:34 CEST by zahra.ak.